Shukrani 2024

Ahsante  veronica mrema 2024



Na Abdusamadu Ninga

Kwa muda mrefu baaada ya kuwasili chuo (UDOM) nilikuwa nikijiuliza, ni lini ndoto yangu itatimia na kuwa mwandishi bora? , Kimsingi ni swali ambalo lililokuwa likigonga kichwani mwangu pasi na kupata majibu hususani nilipohudhuria vipindi darasani na kujifunza mambo mbalimbali ya tasnia yangu.

Nilitamani kupata mtu mwenye uzoefu katika uandishi wa habari hususani makala, achilia mbali kupiga picha kuripoti hali kadhaika kusoma habari kama inavyopaswa kwa mwandishi wa habari aliyekuwa bora.

Siku moja nikiwa nasikiliza ‘lecturer’ darasani DKT. Mary Kafyome alikuwa akisistiza na kueleza ni kwa jinsi gani tutaweza kuwa waandishi bora. Katika mifano yake alikutaja wewe kuwa ni miongoni mwa waandishi wazuri sana Veronica Mrema.

“veronica Mrema ni mwandishi mzuri sana wa masuala ya afya, ninamfuatilia kwa ukaribu sana katika mitandao ya kijamii, nendeni mkajifunze kwa hao watu”

Moja kwa moja, sikuwa na muda wa kupoteza nilikuwa mithili ya mbogo aliyejeruhiwa kwa gobole nikiwa na kiu ya kukufahamu na kujua unafanyaje kazi zako, nilikaa chini na kuyafanyia kazi yale yote aliyotusisitiza mhadhiri wetu Dkt. Kafyome kwa kuanza na kutafuta akaunti yako Veronika mrema katika mtandao wa Instagram, facebook na baadaye kuifahamu Blogu ya M24tzmedia na chaneli ya YouTube M24 Tanzania baada ya kufahamiana nawe.

Mnamo siku ya jumatano tarehe 10 July 2024, kwangu ilikuwa bahati kubwa kupata nambari yako ya simu ili kujifunza kwa ukaribu Zaidi kutoka kwako kupitia mtandao wa instagram, ingawaje nilikuwa nikihofia kukosa nambari yako ya simu kutokana na kasumba iliyopo kwa baadhi ya watu maarufu au waliofanikiwa kwa namna moja au nyigine kutojibu jumbe kutoka kwa watu wanaowafuatilia kwa ukaribu, lakini hukusita na hata ulinipatia nambari yako ya simu na kuahidi kunisadia ili kuwa bora katika uandishi.

Ni vitu gani nimejifunza kwako katika mwaka 2024?

Kuondoa dhana ya ajira kichwani mwangu. umenisistiza sana kuwa ‘upcoming journalist’ wengi huwa na ndoto ya kuajiriwa hali inayopelekea kuvunjika moyo wanapohitimu vyuo.

“upcoming journalist wengi ninaokutana nao huwa na ndoto ya kuajiriwa. Ushauri wangu kwao media industry bongo soko la ajira ni gumu . wanaoajiriwa ni kiduchu mno, muhimu kujipambania kwa kuhakikisha unakuwa bora Zaidi ya wengine” ulinieleza katika ujumbe wa maandishi WhatsApp.

Kuwa tofauti kwa kujifunza sana kuandika habari na kuandika kwa weledi. Ni dhahiri kuwa, utofauti wangu na wanafunzi wengine ni kupitia jitihada kubwa kujifunza na kuandika habari zenye tija ili kujenga uzoefu.

“ndiyo hivyo kijana mwenzamgu, kuwa unique lakini kwa taarifa ambazo zitakupeleka mbali kitaaluma”

Kuandika Makala. kupitia Blogu yako ‘M24tzmedia’ nimekuwa nikifuatilia kwa jicho la kiuandishi na ukaribu Zaidi ili kufahamu ni kwanamna gani nitaweza kuandika kama wewe na hatimaye hata kushinda tuzo mbali mbali iwapo nitashiriki. Hali kadhalika, katika ‘stastus’ yako WhatsApp uliandika kuwa, watu wanahisi tuzo unazopata unapendelewa na kusahau kuwa kuna mambo muhimu yanayopaswa kufanyika wakati wa kuandika ikiwa ni kuchagua wazo lako vizuri, kuandika kwa weledi, kuweka takwimu halisi, kuandika kwa usahihi, vyanzo vya usahihi, kuandika kwa mtiririko mzuri na kushiriki iwapo mashindano yakitangazwa.


Kuwa na moyo wa kujitolea ili kuongeza ujuzi. Kupitia simulizi yako uliyonipatia juu ya maombi yako ya mafunzo Aga Khan university kwa waandishi wa habari za afya, nimejifunza kuwa si vizuri kuacha fursa kwa minajili ya kupata pesa, na wakati mwingine fursa huja baada ya kujitolea. Ulisema kuwa

“ ilitumwa link kwenye group moja la wanahabari nikaingia nikatuma mambi, basi nikaitwa”

Uliendelea kuwa, “..huu nao ni mtihani mwingine kwa wabongo, waliposikia hakuna posho, walikimbia kadhaa. Tukabaki tuliobabi mpaka mwisho, ilikuwa siku 3 ona sasa wamekosa maarifa. Ikiwa wakipata hiyo fursa sijui watalipia dola ngapi”

Uliendelea na kusisitiza kuwa, “ moral of the story ni kwamba usiache fursa ya kuongeza ujuzi kisa haina mshiko”


Mafanikio niliyoyapata badada ya kujifunza kutoka kwako

Kuandika Makala mbali mbali, ikiwemo zinazohusu mazingira na siasa ambazo ni “how would Rufiji wetlands look after three decades from 2024? “ na “ijue kauli mbiu maga na ushindi wa rais Trump”. Lakini pia, niko mbioni kuandika Makala moja inyohusu mchango wa akili mnemba (AI) katika kurahisisha ugunduzi na matibabu ya matatizo ya afya ya akili ikiwa tayari nimendaa data na vyanzo vya uhakika ili kukamilisha Makala hii.

Kushiriki katika mashindano ya “university science competition for Africa 2024”, isivyo bahati sikushinda ingawaje nilipata cheti cha kushiriki mashindano hayo.

Kufanya mahojiano. Moja kati ya vitu ulivyo nisisitiza ili kuwa mwandishi bora ni uwezo wa kufanya mahojiano na watu mbalimbali.

Kupiga picha za stori kwa vitendo.

Graphics.

Malengo ya mwaka 2025 mpaka kufikia februari.

Ninaendelea kujifunza kuendesha vipindi vya redio katika studio iliyopo chuoni na ninatarajia kuendesha vipindi vya redio kwa umahiri ifikapo februari 2025.

Kujifunza kufanya uchambuzi wa data (data analysis and visualisation).

Kimsingi , mwaka 2024 ni mwaka wenye bahati kwangu na ninajivunia sana kukufahamu, kwa minajili nimejifunza vitu vingi sana, ninatoa shukrani zangu za dhati kwako VERONICA MREMA kwa kuwa na moyo na namna hiyo . 

Ahsante!!

.




    

Comments

Popular posts from this blog

Feature