Shukrani 2024

Ahsante veronica mrema 2024 Na Abdusamadu Ninga Kwa muda mrefu baaada ya kuwasili chuo (UDOM) nilikuwa nikijiuliza, ni lini ndoto yangu itatimia na kuwa mwandishi bora? , Kimsingi ni swali ambalo lililokuwa likigonga kichwani mwangu pasi na kupata majibu hususani nilipohudhuria vipindi darasani na kujifunza mambo mbalimbali ya tasnia yangu. Nilitamani kupata mtu mwenye uzoefu katika uandishi wa habari hususani makala, achilia mbali kupiga picha kuripoti hali kadhaika kusoma habari kama inavyopaswa kwa mwandishi wa habari aliyekuwa bora. Siku moja nikiwa nasikiliza ‘lecturer’ darasani DKT. Mary Kafyome alikuwa akisistiza na kueleza ni kwa jinsi gani tutaweza kuwa waandishi bora. Katika mifano yake alikutaja wewe kuwa ni miongoni mwa waandishi wazuri sana Veronica Mrema. “veronica Mrema ni mwandishi mzuri sana wa masuala ya afya, ninamfuatilia kwa ukaribu sana katika mitandao ya kijamii, nendeni mkajifunze kwa hao watu” Moja kwa moja, sikuwa na muda wa kupoteza nilikuwa mithili ...